Mmoja wa haramia hatari wa uwindaji
tembo, anayejulikana kwa jina la “Shetani” amehukumiwa kifungo
cha jela cha miaka 12, nchini Tanzania.
Haramia huyo Boniface Matthew
Maliango anahusika kwa mauji ya maelfu ya tembo, kwa mujibu wa
shirika la moja la uhifadhi wa wanyama pori.
Maliango alikamatwa Jijini Dar es
Salaam Septemba mwaka 2015 baada ya kutafutwa kwa zaidi ya mwaka
mmoja.
Uhalifu wake wa uharamia ulipelekea
kuandaliwa filamu fupi iitwayo The Ivory Game, iliyoongozwa na
muigizaji Leonardo DiCaprio.
Maliango amehukumiwa pamoja na ndugu
zake wa kiume Lucas Mathayo Maliango pamoja na Abdallah Ally Chaoga.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni