Harry Kane amefunga mara mbili na
kuonyesha kiwango cha juu wakati Tottenham iliyopo katika nafasi ya
pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza ikiifunga Everton magoli
3-2.
Mchezaji huyo Muingereza mwenye umri
wa miaka 23 kwa sasa anaongoza kwa ufungaji katika Ligi Kuu ya
Uingereza akiwa na magoli 19.
Kane alifunga goli la kwanza kwa
shuti kali na kisha kuongeza goli la pili katika kipindi cha pili,
kabla ya Romelu Lukaku kuchomoa moja.
Dele Alli aliongeza la tatu katika
dakika ya 90, hata hivyo Enner Valencia naye akatumia dakika chache
zilizosalia kabla ya mpira kuisha kuifungia Everton goli la pili.
Harry Kane akifunga goli lake la pili katika mchezo huo
Romelu Lukaku akifunga goli la kwanza la Everton
Dele Alli akifunga kiufundi goli la tatu la Tottenham
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni