Harry Kane anaweza kuwa nje ya
uwanja katika msimu huu wote baada ya kuumia enka katika mchezo wa FA
ambao Tottenham walishinda kwa magoli 6-0 dhidi ya Millwall.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa
ya Uingereza alitoka katika dimba la White Hart Lane akiwa na
magongo, na kufungwa mguu wake kwa buti la kitabibu.
Kocha wa Spurs Mauricio Pochettino
amelinganisha jeraha alilopata Kane, sawa na alilopata mwezi
Septemba mwaka jana na kumuweka nje ya uwanja kwa wiki saba.
Mguu wa Harry Kane ulioumia ukiwa kati kati ya miguu ya beki wa Millwall
Kiwiko cha mguu wa Harry Kane kikipinda na kuumia baada ya kukaliwa na beki wa Millwall



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni