Paulo Dybala amefunga kwa mikwaju
miwili ya penati wakati Juventus ikiifunga Napoli kwa magoli 3-1
katika mchezo wao wa nusu fainali ya kwanza wa kombe la Coppa Italia.
Alikuwa Jose Callejon aliyewapatia
wageni goli la kuongoza baada ya kufanya shambulizi nzuri, lakini
Muargentina Dybala alisawazisha kwa mkwaju wa penati.
Gonzalo Higuain aliwafungia wenyeji
goli la pili kabla ya baadaye Dybala kuongeza goli la tatu baada ya
kipa Pepe Reina kumuangusha Juan Cuadrado.
Paulo Dybala akifunga goli kwa mkwaju wa penati
Gonzalo Higuain akifunga goli la pili katika mchezo huo



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni