.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 3 Machi 2017

KATIKA KUAZIMISHA SIKU YA WANYAMAPORI DUNIANI,MBIO ZA KUPINGA MAUAJI YA TEMBO ZIITWAZO NDOVU MARATHON KUFANYIKA KESHO JUMAMOSI TAREHE 6/3/2017 KATIKA VIWANJA VYA POSTA KIJITONYAMA:

Kuanzia kushoto ni Meneja Masoko wa Red Bull Bw.Hanson Heddi akifuatiwa na Bw.Amon Mkoga Balozi wa Kupinga mauaji ya Tembo nchini Tanzania na Bw.Boniphace Menchi Meneja wa Usalama kazini wa kampuni ya Puma
 
Je, itakuwaje kama tembo wote nchini Tanzania watakwisha na kubaki tembo mmoja tu? Utafanyaje? Utajisikiaje urithi wetu huu wa kustaajabisha ukipotea katika kizazi chetu? 

Ndo maana Chief Promotions , kwa kwa udhamini wa Puma Energy,D.T Dobie,Songas,EY,Red Bull,Sayona,Colosseum Hotel ingependa ingependa kuutaarifu umma katika kuanzimisha siku ya Wanyamapori Duniani Chief Promotions imeandaa mbio za Ndovu Marathon. 

Mbio hizi zenye lengo la kuongeza ufahamu na kuielimisha jamii kuhusu tatizo sugu la ujangili linaloikabili Tanzania .Mbio hizi zinatarajiwa kuongeza mwamko kwa taasisi za kiraia katika kulinda tembo na wanyama wengine.
 
Tanzania imepoteza asilimia 60 ya tembo wake katika miaka sita iliyopita zaidi kutokana na ujangili kwa ajili ya pembe za ndovu. Wanaonufaika zaidi na pembe za ndovu ni baadhi ya wafanyabiashara haramu wa nchini China na katika nchi nyingine zenye watumiaji wa bidhaa zitokanazo na pembe za ndovu huku Tanzania ikibaki kuwa muathirika wa tatizo hili.
 
“Watalii wengi wanaokuja nchini hupendelea zaidi kuwaona Tembo, na utalii unachangia asilimia 12 ya pato letu la taifa (GDP)”, alisema Amon Mkoga ambaye ni mratibu na Balozi wa Kupinga mauaji ya Tembo Tanzania. “Tembo wetu ni utajiri mkubwa kwa nchi yetu katika njia mbalimbali na serikali yetu imedhamiria kukomesha uhalifu huu. Hata hivyo hatuwezi kufanya jambo hili peke yetu, tunahitaji kupata msaada wa wananchi wote katika jitihada zetu katika kukomesha wizi huu wa urithi wa taifa letu”.
 
Katika utafiti wa hivi karibuni uliohusisha zaidi ya Watanzania 2,000 waishio vijijini na mijini, zaidi ya asilimia 79 walioshiriki walisema kuwa watasikitika endapo tembo watatoweka Tanzania na zaidi ya asilimia 73 walisema wanaamini kuwa tembo ni utambulisho na urithi wa taifa.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya Siku ya Wanyamapori Duniani ni-Tusikilize Sauti za Vijana kwa kuwa mustakabali wa baadae wa Uhifadhi wa wanyamapori ,mimea na mazingira upo mikoni mwao.







Hakuna maoni :

Chapisha Maoni