Akizungumza na mbeyacityfc.com muda mfupi uliopita, afisa habari wa kikosi hiki, Dismas Ten amesema, maandalizi kuelekea mchezo huo yanakwenda vizuri lengo likiwa ni kuhakikisha City inaibuka na ushindi na kujiongezea pointi tatu muhimu hasa baada ya kuvuna pointi moja uwanja wa Taifa jumamosi iliyopita kufuatia sare ya 2-2 na vinara wa ligi, Simba Sc.
Tumeanza mazoezi leo kwa ajili ya mchezo wa jumamosi dhidi ya Ruvu Shooting, ni mchezo muhimu kwetu na hii ndiyo sababu imetufanya kuanza maandalizi na kujipanga vizuri mapema kabisa kuhakikisha tunaibuka washindi, ni wazi utakuwa mchezo mgumu kwa sababu wapinzani wetu si ya kubeza, hatuna wasiwasi kwa sababu tutakuwa tunacheza mbele ya mashabiki wetu ambao watachagiza ushindi kwa ushangiliaji wao.Akiendelea zaidi Ten alisema kuwa kwenye mazoezi ya leo,nyota Ayoub Semtawa,Juma Seif Kijiko na Hussein Ahmed walikosekana mazoezini kutokana na kuwa nje ya jiji la Mbeya kwa matatizo ya kifamilia, huku kiungo Mrisharo Ngassa na Zahoro Pazzi waliobaki jijini Dar baada ya mchezo wa Simba wakijumuika na wezao kujiweka fiti kwa ajili ya mchezo huo wa jumamosi.
Audio Player
00:00
00:00
Download HapaMrisho na Zahoro walibaki Dar baada ya mchezo wa Simba lakini tayari wamewasili Mbeya na leo wamejumuika na wengine kwenye mazoezi ya asubuhi ingawa tumewakosa Semtawa, Kijiko na mlinda lango Hussein Ahmed ambao wako nje ya jiji kwa matatizo ya kifamilia, na imaniyangu kubwa watakuwa wamerejea baada ya siku mbili kutoka sasa.Katika hatua nyingine Ten amedokeza kuwa mlinzi Sankhani Mkandawile aliyeteguka kidole cha mkono wa kushoto baada ya kukanyagwa na Mohamed Huessin kwenye mchezo dhidi ya Simba jumamosi iliyopita amefanyiwa upasuaji na kurejeshwa kwenye sehemu yake kwa kidole hicho kilichokuwa kimefyatuka kabisa.
Sankhani tutamkosa kwa majuma manne kupisha majeraha yake ya kidole cha mkono wa kushoto, alikanyagwa na Mohamed Hussein, tukumbuke kuwa baada ya mchezo ule madaktari wetu walimfanyia matibabu ya awali na tulipofika Mbeya alilazimika kufanyiwa vipimo tena na ikagundulika kuwa kidole chake kilifyatuka kutoka sehemu yake ya kawaida na kuhamia sehemu nyingine hivyo ikalazimu ufanyike upasuaji ili kurejeshwa kwa kidole hicho Dr Guydon Makulila ametufahamisha kuwa upasuaji huo umefanikiwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni