Celtic imefikisha rekodi ya kucheza
mechi 22 za Ligi Kuu ya Scotland bila ya kufungwa na kuongoza kwa
tofauti ya pointi 27, ikihitaji pointi saba tu kutwaa ubingwa kwa
mara sita mfululizo.
Katika mchezo huo wa jana dhidi ya
Inverness, Celtic iliutawala mpira lakini ilibidi ingojee hadi katika
dakika ya 43 ya mchezo, kabla ya Scott Sinclair kufunga goli zuri la
shuti la kuzungusha.
Goli lao la pili lilipatikana katika
sekunde ya 12 ya kipindi cha pili baada ya Moussa Dembele
akitumbukiza kimiani kwa mpira.
Stuart Armstrong alifunga goli kwa
mpira wa adhabu na kisha Dembele akafunga goli lake la pili na la nne
katika mchezo huo na kufanya matokeo kuwa 4-0.
Moussa Dembele akifunga goli kwa kuubetua kidogo mpira juu


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni