Mwanamke wa Misri anayeaminika kuwa
mtu mnene kuliko wote duniani akiwa na kilo 500 anaendelea na
upasuaji wa kumpunguza unene nchini India.
Msemaji wa hospitali la Mumbai ya
Saifee, amesema mwanamke huyo Eman Ahmed Abd El Aty, 36,
ameshapunguza kilo 100 tangu awasili India mwezi Januari.
Familia yake imesema kuwa Eman
hakuwahi kutoka nyumbani kwake kwa muda wa miaka 25, isipokuwa siku
aliyosafirishwa kwenda Mumbai kwa matibabu.
Mwanamke Eman Ahmed Abd El Aty kabla ya kufanyiwa upasuaji na kupunguzwa kilo 100
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni