Baada ya kusimama kwa muda wa takribani wiki tatu kupisha michuano mbalimbali ya kimataifa kwa ngazi ya timu ya taifa na klabu, kadhalika michuano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inarejea tena kesho Jumamosi kwa michezo miwili.
Michezo ya kesho Jumamosi Aprili mosi, mwaka huu itakuwa kati ya Mabingwa watetezi wa VPL, Young Africans na Azam - mechi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mbeya City na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mechi zote za Jumamosi, zitafanyika saa 10.00 jioni.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
http://tff.or.tz/news/840-mzunguko-wa-25-ligi-kuu-ya-vodacom
GHANA KUTUA, SERENGETI BOYS KUIVAA TENA BURUNDI
Timu ya taifa ya vijana ya Ghana wenye umri wa chini ya umri wa miaka 17 maarufu kwa jina la Black Starlets, inatarajiwa kutua kesho Jumamosi Aprili mosi saa 9.40 usiku kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya wenyeji Serengeti Boys ambayo ni timu ya taifa ya vijana ya Tanzania.
Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa, kati ya wageni The Black Starlets na Serengeti Boys unatarajiwa kufanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam saa 10.00 jioni. Timu hiyo itafikia Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
http://tff.or.tz/news/839-ghana-kutua-serengeti-boys-kuivaa-tena-burundi
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni