Sergio Ramos ameifungia Real Madrid
goli la ushindi la dakika za mwisho na kuifunga Real Betis iliyobakia
na wachezaji 10 kwa magoli 2-1 katika mchezo wa La Liga.
Katika mchezo huo Keylor Navas
alikoswakoswa kupata kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Darko Brasanac,
kisha baadaye akajifunga kwa mpira wa shuti la Antonio Sanabria.
Mchezaji nyota wa Real Madrid
Cristiano Ronaldo aliifungia Madrid goli la kusawazisha kupitia kwa
krosi ya Marcelo kabla ya mapumziko.
Beki wa Real Betis, Matteo Piccinini
alitolewa nje kwa kumchezea vibaya Lucas Vazquez zikiwa zimebakia
dakika 12, kabla ya Ramos kufunga kwa kichwa mpira wa kona ya Toni
Kroos.
Keylor Navas akiwa amelala chini baada ya kufanya uzembe na kujifunga
Mpira wa kichwa cha kuchupa kilichopigwa na Ronaldo ukimshinda kipa na kujaa wavuni
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni