Liverpool imepata ushindi muhimu
katika kuwania nafasi nne za juu za Ligi Kuu ya Uingereza baada ya
kuifunga Arsenal kwa magoli 3-1 katika mchezo uliochezwa kwenye dimba
la Anfield.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger,
alifanya kosa la kumuanzisha benchi Alexis Sanchez ambaye ni kinara
wao wa kupachika magoli aliyekwisha funga magoli 17 katika mchezo ya
Ligi Kuu ya Uingereza.
Roberto Firmino alifunga goli la
kwanza na kisha Sadio Mane akafunga goli tamu la pili kabla ya
mapumziko. Sanchez alitokea benchi katika kipindi cha pili na
kumtengenezea goli Danny Welbeck, kabla ya Georginio Wijnaldum
kufunga goli la tatu dakika za majeruhi.
Danny Welbeck akifunga goli pekee la Arsenal katika mchezo huo
Msenegal Sadio Mane akifunga goli la pili la Liverpool
Georginio Wijnaldum akifunga goli la tatu katika dakika za mwisho
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni