Mhandisi Abdallah Mziray (mwenye koti la udhurungi), akieleza jitihada zinazofanywa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) za kuhamisha mto Kimilagabalu unaosababisha mafuriko kwenye njia ya kutua na kuruka kwa ndege kipindi cha mvua kubwa.
Ujenzi wa jengo la kuongozea ndege la Kiwanja cha ndege cha Mwanza, ukiendelea, ambapo unatarajiwa kukamilika baadaye mwaka huu. Mnara huu umeelezwa utakuwa na kiwango cha juu cha mawasiliano kwa nchi za Afrika Mashariki
Jengo jipya la kuhifadhi mizigo la kiwanja cha ndege cha Mwanza, likiendelea na ujenzi wake, jengo hilo linaukubwa wa mita za mraba 1500
Mizigo ya mabaki ya samaki aina ya Sangara maarufu kama mabondo yakiwa kwenye Kiwanja cha ndege cha Mwanza yakisubiri kusafirishwa nchini China kupitia Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo hutumika kutengeneza nyuzi zinazotumika kushona wagonjwa kwenye hospitali.
Mwanzo wa ujenzi wa daraja la kuunganisha barabara ya kiungio cha ndege za mizigo na barabara ya kutua na kuruka ndege, ambayo itawezesha ndege za mizigo kuelekea kwenye jengo jipya la mizigo.
Afisa Usalama wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, Juma Nyamhanga (kushoto) akimfafanulia mmoja wa abiria ujazo anaotakiwa kusafiri nao kwa chupa za mafuta na manukato mbalimbali, kama alivyoishika pichani. Ujazo unaotakiwa kwa abiria kusafiri nao katika begi la mkononi ni kuanzia ujazo wa 50-100, na ikizidi lazima uingie kwenye begi litakaloingia sehemu ya mizigo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni