.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 28 Machi 2017

UWANJA WA TIMU YA CARLOS TEVEZ WAUNGUA MOTO


Uwanja wa timu ya Ligi Kuu ya China ya Shanghai Shenhua iliyogonga vichwa vya habari kwa kumsajili Carlos Tevez kwa mshahara wa paundi 615,000 kwa wiki, umeungua moto.

Miale ya moto pamoja na moshi mzito umeonekana katika sehemu ya uwanja huo wa Hongkou wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 33,000 leo asubuhi.

Picha zilizopigwa kwa simu zinawaonyesha askari wa kikosi cha zimamoto wakikabiliana na moto huo mkubwa ulioanza majira ya saa mbili na nusu asubuhi.
                        Moto ukiwa unateketeza sehemu ya uwanja wa timu ya Shanghai Shenhua
                                          Vikosi vya zimamoto vikipambana kuuzima moto huo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni