Arsenal imefufua matumaini ya
kutinga Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani baada ya kupata ushindi wa
magoli 3-0 dhidi ya West Ham na kukwea hadi nafasi ya tano katika
Ligi Kuu ya Uingereza.
Baada ya kipindi cha kwanza ambacho
hakikushuhudia goli, Mesut Ozil akiichezea Arsenal kwa mara ya 150
aliifungia goli la kwanza kufuatia makosa ya kutomiliki mpira ya Jose
Fonte.
Ozil aligongeana vyema na Alexis
Sanchez na kumtupia krosi Theo Walcott ambaye alikuwa kapteni
kufuatia Laurent Koscielny, ambaye hakufanya ajizi na kufunga goli.
Olivier Giroud aliyetokea benchi
kuchukua nafasi ya Alex Oxlade-Chamberlain, alipiga shuti la
kuzungusha na kufunga goli la tatu.
Mesut Ozil akiwa ameupiga mpira uliozaa goli la kwanza
Olivier Giroud akipiga shuti la kuzungusha na kufunga goli la tatu la Arsenal
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni