Bondia Anthony Joshua amechezea
vizuri pambano la jana usiku na kujiongezea mkanda wa uzito wa juu wa
WBA huku akiwa na mkanda wa IBF, baada ya kumtoa KO bondia Wladimir
Klitschko katika pambano lililofanyika kwenye dimba la Wembley.
Katika pambano hilo lililoshuhudiwa
na mashabiki 90,000, bondia Joshua alimuangusha chini Klitschko
katika raundi ya tano kabla ya yeye pia kuangushwa chini kwa mara ya
kwanza kati ya mapambano yake 19 katika raundi ya sita ya mchezo huo.
Mabondia hao wate wawili walionekana
kuwa ni hatari katika raoundi mbili za mwanzo ambazo hazitosahaulika
katika kumbukumbu za ngumi, kabla ya Joshua kumsimamisha Klitschko
katika raundi ya 11.
Bondia Anthony Joshua akimshindilia ngumi bondia Wladimir Klitschko
Bondia Wladimir Klitschko akiwa ameenda chini huku refa akimzuia Anthony Joshua asilete maafa zaidi
Bondia Anthony Joshua akiwa chini baada ya kupigwa ngumi nzito na bondia Wladimir Klitschko
Bondia Anthony Joshua akiwa amempa konde lililomuingia barabara bondi Wladimir Klitschko
Bondia Anthony Joshua akishangilia baada ya kumdunda bondi Wladimir Klitschko aliyechini
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni