Timu ya Chelsea imeendelea kujikita
kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza kwa tofauti ya pointi saba baada
ya kupata ushindi mzuri wa magoli 4-2 dhidi ya Southampton katika
dimba la Stamford Bridge.
Katika mchezo huo Eden Hazard na
Diego Costa walishuka katika kikosi cha kwanza na ilimchukua dakika
tano tu Hazard kuifungia Chelsea goli la kwanza, lakini mchezaji wa
zamani wa Chelsea Oriol Romeu alisawazisha goli hilo.
Gary Cahill aliifungia Chelsea goli
la pili na kisha Diego Costa akaongeza goli la tatu katika dakika ya
53 na kufunga la nne dakika ya 89, kabla ya mchezaji mwingine wa
zamani wa Chelsea Ryan Bertrand kuifungia Soumpton goli la pili
katika dakika ya 90+4.
Eden Hazard akiifungia Chelsea goli la kwanza katika mchezo huo
Mshambuliaji nyota Diego Costa akifunga goli la tatu la Chelsea
N'Golo Kante akimchezea rafu Ward-Prowse na kujikuta akiambulia kadi ya njano




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni