Chelsea inaongoza kwa tofauti ya
pointi saba kileleni dhidi ya Tottenham baada ya kupambana mno kupata
ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Manchester City.
Kwa kipigo hicho kikosi cha Pep
Guardiola kimekubali kipigo cha nyumbani na ugenini kutoka kwa
Chelsea kwa mara ya kwanza chini ya kocha huyo.
Katika mchezo huo Eden Hazard
aliipatia Chelsea goli la kuongoza katika dakika ya 10 baada ya shuti
alilopiga kumgonga Vincent Kompany na kumpita kipa Willy Caballero.
Kipa wa Chelsea Thibaut Courtois
alifanya kosa katika kuokoa na kutoa mwanya kwa David Silva
kumtengenezea nafasi ya kufunga Sergio Aguero.
Fernandinho alimchezea rafu Pedro na
kutolewa penati ambayo licha ya kipa Cabellero kuiokoa penati
iliyopigwa na Hazard, mpira ulimrudia na akatumbukiza la pili.
Kipa wa Manchester City Willy Caballero akichanganyikiwa baada ya kufungwa
Sergio Aguero akishangilia baada ya kufunga goli pekee la Man City
Nayo Tottenham imetokea nyuma
kufungwa goli 1 katika dakika ya 11 na kubadili matokeo katika dakika
za mwisho kwa kufunga magoli matatu katika dakika za 88, 90 na 94 na
kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Swansea City.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni