Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim Haji kati kati aliyevaa Suti nyeusi akikiongoza Kikao cha maandilizi ya kuanzishwa mafunzo maalum ya kinga ya msingi Maskulini kwa lengo la kutoa elimu itakayowasaidia wanafunzi kujikinga dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya.
Mshauri wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mapambano dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya { UNODC } Bibi Sylvie Bertrandwa Pili kutoka kushoto akifafanua jambo juu ya mpango huo utakaosimamiwa na UNODC.
Uongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mapambano dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya { UNODC } umeamua kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuanzisha mafunzo maalum ya kinga ya msingi Maskulini kwa lengo la kutoa elimu itakayowasaidia kujikinga dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya.
Uongozi huo umekutana na Watendaji wa Tume ya Udhubiti wa Dawa za Kulevya pamoja na wale wanaosimamia udhibiti wa uhalifu Chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim Haji Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Mshauri wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mapambano dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya { UNODC } Bibi Sylvie Bertrand alisema mpango huo wa Mafunzo utashirikisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.
Bibi Sylvie alisema katika kuupanguvu zaidi mpango huo ili ufanikiwe vyema Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto pia itakuwa mshirika katika mpango huo utaoratibiwa na Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Zanzibar.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
6/4/2017.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni