Klabu moja ya usiku nchini Tunisia
imefungwa baada ya picha za video kumuonyesha DJ akichanganya muziki
na sauti ya adhana ambayo hutumika kuita watu kwenda kuswali.
Video hiyo iliyosambazwa Jumapili
kutoka katika tamasha la Orbit Festival kaskazini mashariki mwa mji
wa Nabeul ililalamikiwa mno kwenye mitandao ya jamii..
Gavana wa Nabeul, Mnaouar Ouertani,
amesema klabu hiyo itaendelea kufungwa hadi hapo itakapotolewa kauli
nyingine. Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni