.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 26 Aprili 2017

MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM YAOMBWA KULINUSURU DARAJA LISISOMBWE NA MAFURIKO

Wakazi wa Gongolamboto wakipita katika daraja ambalo kingo zake zimesombwa na mafuriko barabara ya kuelekea Machinjio ya Pugu Kajiungeni Dar es Salaam leo.
                Mwonekano wa eneo hilo baada ya kingo kusombwa na maji ya mafuriko
            Daladala likipita kwenye daraja hilo ambalo kingo zake zimesombwa na mafuriko

Na. Mtandao wa Habari za Jamii 

MANISPAA ya Ilala imeombwa kufanya jitihada za makusudi kuinusuru daraja linaloungani eneo la Gongola mboto na Machinjio ya Pugu ambalo lipokatika hatari ya kusombwa na maji.

Wito huo umetolewa Dar es Salaam leo na wakazi wa Pugu Machinjioni ambao wamesema iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa mawasiliano kati ya wananchi wa eneo hilo na Gongolamboto yatatoweka hivyo kuwa adha kwao kwa kufika makwao kwa kupitia Pugu Kajiungeni badala ya barabara ya Gongo lamboto Pugu Machinjioni kupitia kiwandacha kutengeneza nguo cha Namera.

Tunaomba manispaa yetu ilifanyie ukarabati daraja hili ambapo kwa sehemu kubwa kingo zake zimesombwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha " alisema Omari Mshamu mkazi wa eneo hilo.

Mkazi mwingine wa eneo hilo Marietha Stanslaus alisema iwapo daraja hilo linasombwa na maji watakaopata shida zaidi ni wanafunzi kwani watalazimika kutumia njia ndefu kufika mashuleni kwao kutokana kuwa wengi wao wanasoma shule za Gongolamboto.

Jithada za kumpata diwani wa eneo hilo ili kuzungumzia suala hilo zilishindika baadaya kupiga simu yake ambayo haikupatikana. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba (0712-727062)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni