Bingwa wa Olimpiki na mbio za
marathoni za London Mkenya Jemima Sumgong amekuwa manariadha wa Kenya
wa hivi karibuni kubainika kutumia dawa za kusisimua misuli.
Mwanariadha huyo mwenye miaka 32
amebainika kutumia dawa iliyopigwa marufuku michezoni ya EPO, vipimo
vya akiwa kwenye mashindano na nje ya mashindani vya bodi ya IAAF
vimeonyesha
Mkenya Sumgong ni mwanariadha wa
kwanza wa kike Kenya kushinda medali ya dhahabu katika mbio za
Olimpiki, na alikuwa anatarajiwa kutetea taji lake la mbio za
marathoni za London Aprili 23.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni