Kipa wa Manchester United David De
Gea amechochea uvumi zaidi unaomuhusisha na kuhamia klabu ya Real
Madrid baada ya kutangaza kuuza jumba lake lililopo katika Jiji la
Manchester.
Kipa huyo Mhispania aliyejiunga na
United akitokea Atletico Madrid mwaka 2011, amekuwa mara kwa mara
akihusishwa na mpango wa kurejea nchini kwao, ambapo mwaka 2015
alishindwa kuhama kutokana na makosa ya kimkataba.
Uvumi wa uwezekano wa De Gea kurejea
Hispania haujamalizika, hii ni baada ya gazeti la The Sun kuripoti
kuwa kipa huyo ameliweka sokoni jumba lake lenye thamani ya paundi
milioni 3.85.
Jumba la David De Gea analodaiwa kuliuza lenye thamani ya paundi milioni 3.85


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni