Mchezo wa kimataifa wa Raundi ya
Pili kati ya Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na Mouloudia
Club D’Alger ya Algeria unatarajiwa kufanyika leo Jumamosi Aprili
8, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam ambako
utachezeshwa na waaamuzi kutoka Rwanda.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), waamuzi hao ni Louis
Hakizimana ambaye atakuwa mwamuzi wa kati akisaidiwa na Theogene
Ndagijimana akiwa mshika kibendera wa mstari wa kulia na Jean Bosco
Niyitegeka ambaye atakuwa mshika kibendera mstari wa kushoto.
Mchezo huo muhimu kwa Young Africans
kusonga mbele kama ilivyotokea msimu uliopita kwa kuifunga Sagrada
Esperanca ya Angola na kutinga hatua ya makundi, viingilio vimepangwa
kuwa Sh 30,000 kwa VIP ‘A’; Sh 20,000 kwa VIP ‘B’ na ‘C’
wakati mzungunguko itakuwa ni Sh 5,000.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni