.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 25 Aprili 2017

WAZIRI MKUU AKAGUA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MUUNGAN


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ukaguzi wa miundombinu kwa ajili ya sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kusema kuwa maandalizi yake yako pazuri.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Aprili 24, 2017) mara baada ya kupokea taarifa ya maandalizi na kukagua Uwanja wa Jamhuri ambapo sherehe hizo zitafanyika na uwanja wa Nyerere Square ambako zitafanyika burudani mbalimbali kama sehemu ya maadhimisho hayo.

“Nilikuja kuangalia maandalizi ya sherehe hizo yamefikia wapi, najua kutakuwa na maonyesho ya kijeshi zikiwemo michezo na burudani kutoka Tanzania Bara za Visiwani,” alisema.

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wakazi kutoka wilaya zote za mkoa wa Dodoma na mikoa ya jirani wafike kwenye maonyesho hayo ambayo kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania yanafanyika mkoani humo.

“Tunatarajia wageni wengi kutoka nje ya mkoa huu wakiwemo viongozi wastaafu wa kitaifa, waheshimiwa mabalozi na wake wa waasisi wa Taifa hili, Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume. Pia tutawatambulisha rasmi ndugu zetu waliochanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964,” alisema.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba sehemu zilizobakia zitakamilika kabla ya kesho.

IMETOLEWA NA: 

OFISI YA WAZIRI MKUU, 
S. L. P. 980, 
DODOMA. 
JUMATATU, APRILI 24, 2017.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni