Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza juzi.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) pamoja na meza kuu kwenye maadhimisho hayo akizinduwa taarifa ya "So This Is Democracy" ya MISA TAN kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani zilizofanyika kitaifa mkoani Mwanza juzi. Anaye msadia kushoto ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya MISA TAN.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe pamoja na viongozi mbalimbali waliopo meza kuu wakionesha baadhi ya nakala za taarifa ya "So This Is Democracy" ya MISA TAN mara baada ya kuzinduliwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani zilizofanyika kitaifa mkoani Mwanza juzi.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Tanzania, Salome Kitomari akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Mwakyembe kuzungumza kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza juzi.
Mwanachama wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho akizungumza kuwasilisha ujumbe wa TAMWA kwenye kongamano hilo la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza juzi.
Mwakilishi wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez akizungumza katika kadamnasi hiyo.
WAZIRI wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema
wizara hiyo inaharakisha kukamilisha kwa kanuni zitakazo simamia
mitandao ya kijamii inayoendesha shughuli zake kama vyombo vya habari
vya kieletroniki (Tv na Redio).
Waziri
Dk. Mwakyembe aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wadau
mbalimbali wa vyombo vya habari na wanataaluma wa vyombo vya habari
katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani
zilizofanyika kitaifa mkoani Mwanza.
"Hii
media nyingine hii ambayo inafanya kazi zilezile kama za vyombo vya
habari vya eletroniki, lakini nadhani tulikuwa hatujaamka kutunga
kanuni, lakini nauhakika ndani ya muda si mrefu hilo
litafanyika...lakini litakuwa zoezi shirikishi kama nilivyo ahidi...,"
alisema Waziri Dk. Mwakyembe.
Hata
hivyo aliwataka wananchi kutumia taarifa za kwenye mitandao kwa
tahadhari na kama tetesi ili kuondoa mikanganyiko ambayo imekuwa
ikitokea kwenye mitandao hiyo.
Kwa
upande wake Mtaalamu wa Mawasiliano, Innocent Mungy akiwasilisha mada
ya 'Mchango wa Mitandao ya Kijamii katika kukuza Uhuru wa Kujieleza'
kwenye kongamano hilo ilisema mitandao ya kijamii kupitia intaneti
imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya mawasiliano licha ya uwepo wa
changamoto zake.
Alisema
mitandao kama blogu imekuwa ikisambaza taarifa kwa kiasi kikubwa na
kutumiwa na idadi kubwa ya watu nchini katika kupata taarifa. "Bloggers
wamekuwa sehemu kubwa ya mawasiliano...hadi taasisi mbalimbali zimeona
umuhimu wake nazo zimeingia na kuwa zikitumia mitandao hiyo katika kutoa
taarifa...," alisema mtaalamu huyo wa mawasiliano nchini.
Akifafanua
alisema kutokana na wimbi la kukua kwa mitandao hiyo na kusambaza
taarifa wakati mwingine imekuwa vyanzo vya taarifa hata katika vyombo
rasmi vya habari. Alisema licha ya mafanikio hayo mitandao hiyo imekuwa
na changamoto kubwa ikiwepo uwepo wa taarifa za uongo kupitia mitandao
hiyo, matumizi mabaya ya mitandao hiyo.
Aidha
akijibu moja ya swali lililoulizwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki
wa Mitandao ya Kijamii (TBN) juu ya mvutano wa mitandao ya kijamii
'Blogu' na vyombo rasmi vya habari kuchukuliana taarifa basipo utaratibu
kwa pande zote, alizitaka pande zote kukaa na kuzungumza kwa pamoja
kuangalia namna zinaweza kutatua mvutano huo wa chini chini kwa
maendeleo zaidi ya tasnia.
"...Nianze
kwa kupongeza kuwa kwa sasa bloga wanavyofanya kazi kunamabadiliko
makubwa ukilinganisha na hapo nyumba, sasa hivi hadi wao (bloggers)
wanaumoja wao unaowaunganisha (TBN). Kaeni chini mzungumze naamini
mtayamaliza, mnaweza kuwatumia hata waandishi wa habari wakongwe na hata
bloga wazoefu ili kumaliza mgogoro huo wa chini chini na vyumba vya
habari," alisema.
Hata
hivyo alisema kuwa mitandao ya kijamii sio mibala bali watumiaji wake
ndio wabaya na kuongeza mitandao hiyo imekuja na mabadiliko makubwa
katika sekta ya mawasiliano.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni