.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 25 Mei 2017

MANCHESTER UNITED WATWAA UBINGWA WA LIGI YA UROPA

Manchester United imetwaa kumbe la pili kubwa katika msimu huu na kufanikiwa kutinga katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuifunga Ajax magoli 2-0 na kushinda Ligi ya Uropa Jijini Stockholm.

Katika usiku uliojawa huzuni kufuatia shambulizi lililouwa watu 22 katika tamasha la mwanamuziki Ariana Grande katika ukumbi wa Manchester Arena jumatatu mashabiki wa Manchester United walilazimika kutoshangilia kupitiliza.

Manchester United ilipata goli la kwanza kupitia shuti la Paul Pogba lililogongwa na kumpoteza uelekeo goli kipa katika dakika ya 18 na kisha baadaye Henrikh Mkhitaryan akafunga goli lake la sita katika michuano hiyo akiunganisha mpira wa kona uliopigwa kichwa na Chris Smalling.
                 Mpira uliopigwa na Paul Pogba ukimshinda kipa wa Ajax na kujaa wavuni 
               Henrikh Mkhitaryan akiangalia mpira alioupiga ukielekea kujaa wavuni
         Kocha Jose Mourinho akinyanyuliwa juu na timu yake ya ufundi baada ya ushindi

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni