
Wageni wa meza kuu wakifurahia jambo wakati wa kuanza kwa fainali ya mashindano ya Habibu cup katika uwanja wa Cleopa Msuya wilayani Mwanga. Kikosi cha timu ya Kifaru kikipasha misuli joto. Kikosi cha timu ya Nyerere kikipasha misuli joto. Mgeni rasmi katika mchezo wa fainali za Mashindano ya Habibu Cup ,Thabit Mndeme akisalimiana na wachezaji wa timu ya Nyerere. Mgeni rasmi katika mchezo wa fainali za Mashindano ya Habibu Cup ,Thabit Mndeme akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kifaru. Mgeni rasmi katika mchezo wa fainali kati ya timu za sekondari za Nyerere na sekondari ya Kifaru,Thabit Mndeme akizungumza kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali baina ya timu hizo mbili.
Kikundi cha ushangiliaji cha timu ya Nyerere .
Kikundi cha ushangiliaji cha timu ya Kifaru.
Sehemu ya hekaheka katika mchezo huo wa fainali.
Mchezaji wa timu ya Sekondari ya Kifaru akipiga penati iliyopelekea ushindi wa jumla ya bao 5 kwa 3 kwa timu ya Kifaru katika mchezoo wa fainali dhidi ya timu ya sekondari ya Nyerere .
Baadhi ya mashabiki walijitokeza kushuhudia michezo ya fainali katika mashindano hayo.
Mgeni rasmi Zuhura Mndeme akielekea katika uwanja wa mchezo wa Netiboli kwa ajili ya ufunguzi ya kuanzisha fainali ya mchezo huo kati ya timu ya Green Bird Collage na Sekondari ya Usangi Girls Day.
Timu ya Netiboli ya Shule ya sekondari ya Usangi Girls Day
Timu ya Green Bird Collage.
Mgeni rasmi kwa upande wa mchezo wa Netiboli ,Zuhura Mndeme akisalimiana na wachezaji wa timu ya Green Bird Collage.
Mgeni rasmi kwa upande wa Netiboli,Zuhura Mndeme akisalimiana na wachezaji wa timu ya Sekondari ya Usangi Girls Day.
Mwamuzi wa mchezo huo wa fainali akimkaribisha mgeni rasmi Zuhura Mndeme kufungua rasmi mchezo huo wa fainali.
Mgeni Rasmi Zuhura Mndeme akirusha mpira kwenye mlingoti wa goli wakati wa ufunguzi rasmi wa mchezo wa faiali ya Netiboli.
Mchezo wa fainali ukiendelea baina ya timu ya Green Bird Collage na Sekondari ya Usangi Girls Day mchezo uliomalizika kwa timu ya Green Bird kutangazwa malkia mpya wa mchezo huo baada ya kushinda kwa point 17 kwa 15 za Usangi Girls.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni