.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 1 Mei 2017

SMZ YAAHIDI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA ZANUSO KATIKA SEKTA YA UJASIRIAMALI

Mshiriki wa Mashindano ya ujasiriamali kwa Vyuo vikuu, Tahani Said akipokea zawadi kutoka kwa Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Viwanda Zanzibar, Saleh Suleiman Hamad katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar(ZANUSO).
Mshiriki wa Mashindano ya ujasiriamali kwa Vyuo vikuu, Issah Eugenio ambaye mradi wake wa Handbags made in Jeans umechukua nafasi ya mwanzo, akipokea zawadi kutoka kwa Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Viwanda Zanzibar, Saleh Suleiman Hamad katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar(ZANUSO).
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Viwanda Zanzibar, Saleh Suleiman Hamad akiutubia wakati wa kufunga mashindano yaliyoandaliwa na jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar(ZANUSO) huko ZU kampasi kuu ya Tunguu.
Mlezi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar(ZU), Mhadhiri wa Chuo hicho Juma Rashid Khamis wakati akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya miradi ya Ujasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu Zanzibar yaliyofanyika katika kampasi ya chuo hicho huku Tunguu, Unguja.
Mkurugenzi wa Kampuni ya SISI Consultants, Mohamed Wario ambayo ni miongoni mwa wadhamini akitoa nasaha zake kwa wanafunzi walioshiriki katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar(ZANUSO) huko ZU kampasi kuu ya Tunguu.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mashindano hayo pamoja na Viongozi wa ZANUSO na ZU pamoja na mgeni rasmi.

                                                                                              Na Juma Farid, Zanzibar.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na baadhi ya Jumuiya za wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini zinazoonyesha nia ya kuthamini fani ya Ujasiriamali kama chanzo mbadala cha kupunguza tatizo la Ajira nchini.

Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Viwanda Zanzibar, Saleh Suleiman Hamad kwa Niba ya Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali Wakati akifunga warsha ya Mashindano ya miradi ya Ujasiriamali kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Zanzibar yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar ( ZU) huko Kampasi Kuu ya Chuo hicho Tunguu.

Amesema ubunifu ulionyeshwa na wanafunzi hao katika uandishi, mikakati na bidhaa za miradi ya Ujasiriamali waliyoiwasilisha katika Mashindao hayo inajenga ushawishi kwa serikali na mashirika mengine ya kimataifa kuwaunga mkono ili wafikie malengo yao ya kujiajiri na kuwaajiri vijana wengine wasiokuwa na ajira.

Amesema bado wanafunzi wengi wanaohitimu elimu ya ngazi ya vyuo vikuu nchini hawajatumia fursa zinazopatikana katika fani ya Ujasiriamali ambayo imekuwa ikitegemewa na mataifa mbali mbali duniani kupunguza tatizo la ajira hasa kwa vijana.

“ Nasaha zangu kwenu kabla ya kuanzisha mradi wowote fanyeni tathimini na utafti wa kitaalamu kubaini aina ya ujasiriamali unaotaka kufanya una maslahi gani na wateja wako wahitaji bidhaa za aina gani sambamba na kuwa wabunifu wa kufanya miradi isiyofanana.”, alisema Katibu huyo.

Aidha alieleza kwamba kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Masoko, Balozi Amina Salum Ali serikali itaendelea kudhamini miradi itakayoonyesha ustawi na maendeleo endelevu.

Pia katika juhudi za kuwajengea uwezo wajasiriamali hao alieleza kwamba serikali itashawishi makampuni na mashirika ya kimaita ya kibiashara kufanya kazi kwa karibu na jumuiya hizo ili zipate soko la uhakika la kuuzia bidhaa zao.

Hata hivyo ametoa nasaha zake kwa wajasiriamali hao kutengeneza bidhaa bora zitakazokubalika katika soko la kimataifa pamoja na kujiongeza kitaaluma kupitia mafunzo mbali mbali ya fani hiyo.

Mapema akizungumza Mlezi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar(ZU), Bw. Juma Rashid Khamis ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo hicho aliwasihi washiriki wa mashindao hayo kuendelea kujifunza zaidi kupitia kwa wajasiria mali wakongwe ili wapate ujuzi wa ziada wa kukabiliana na ushindani wa bidhaa na miradi ya ujasiriamali ndani na nje ya Zanzibar.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya SISI Consultants, Mohamed Wario aliwataka Wasomi hao kutumia vizuri fursa hiyo ya ujasiria mali kwa kuangazia sehemu tofauti ambazo bado hazijatumiwa vizuri kibiashara zikiwemo Sekta ya Utalii, Uvuvi na Ufugaji ili kuzalisha bidhaa bora zinazotokana na rasilimali hizo na kuzishindanisha katika soko la ndani na nje ya nchi.

“ Kampuni ipo tayari kushirikiana na nyinyi wakati wowote lakini lazima mjiongeze zaidi kufikia lengo la kufanya miradi bora na inayoendana na mahitaji ya sasa ili mpate mafanikio zaidi”, alisisitiza Mkurugenzi huyo.

Kwa upande wake mshiriki wa mashindano hayo aliyeshindanisha mradi wa usindikaji wa bidhaa aina ya Jam inayotumia kwa chakula cha mkate iliyotengenezwa kwa matunda ya Maembe, Ehlam Ali Khamis alisema wazo la kutengeza bidhaa hizo ni kutokana na kukosekana kwa matumizi mazuri ya matunda hayo hasa wakati wa msimu wake hali inayosababisha kuharibika kwa kukosekana kwa viwanda vya kusindika matunda hayo.

Akitoa ufafanuzi juu ya Warsha hiyo, Mwanzilishi na Msimamizi wa Mashindano hayo Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Zanzibar ZANUSO, Mohamed Omar alifafanua kwamba awali mchakato huo ulishirikisha jumla ya vyuo Sita na ulipopita mchujo vikabaki vitatu ambavyo ni Zanzibar University (ZU), State University of Zanzibar(SUZA) na Summait University.

Mashindano hayo wamepatikana washindi saba ambao wamepewa Zawadi mbali mbali zikiwemo simu za Adroid, lakini nafasi ya kwanza ambayo imeshikiliwa na Issah Eugenio kwa mradi wa Handbags Made in Jeans, nafasi ya pili ni Ehlam Ali Khamis kwa mradi wa Mango Jam na Tatu Ibrahim ahmad abdalla na Sabrina Khamis Machano wa mradi wa Teke knowlge solutions company wote kutoka vyuo tofauti vilivyoshiriki kwa awatua hiyo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni