.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 4 Mei 2017

WAZIRI KIJANA ZAIDI NCHINI SOMALIA AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI

Waziri wa Ujenzi wa nchini Somalia Abdullahi Sheikh Abas ameuwawa baada ya msafara wake kushambuliwa Jijini Mogadishu.

Taarifa zinasema kwamba Waziri Abdullahi Sheikh Abas, alipigwa risasi na kufa karibu na Ikulu ya rais kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Somalia.

Bw. Abas aliwahi kuwa mkimbizi aliyekulia kambi ya Dadaab nchini Kenya, ambayo ni makazi ya mamia ya wasomali waliokimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Alikuwa mbunge kijana kuliko wote katika nchi hiyo Novemba mwaka jana, akiwa na miaka 31 alipomshinda waziri wa zamani.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni