.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 10 Juni 2017

TIMU YA CLEVELAND CAVALIERS YAIFUNGA GOLDEN STATE WARRIORS

Timu ya Cleveland Cavaliers imefufua matumaini katika michezo ya fainali ya NBA baada ya kuinyima ushindi Golden State Warriors baada ya kuibuka na ushindi waliokuwa wakiuhitaji katika mchezo wa fainali ya nne.

Katika mchezo huo wa jana mabingwa hao watetezi Cleveland waliibuka na ushindi wa pointi 137-116, matokeo yanayoifanya Warriors kuongoza kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Cavaliers.

Katika mchezo huo ulioshudiwa na mastaa kibao Kyrie Irving alifunga pointi 40 huku LeBron James akifunga pointi 31 na kumaliza ubabe wa Golden State Warriors wa kuwafunga katika michezo mitatu ya awali ya fainali.

Hata hivyo Golden Sate Warriors wanaweza kuutwa ubingwa wa NBA nyumbani watakapokutana tena katika mchezo wa tano wa fainali siku ya jumanne.
                            Lebron James akiruka juu na kufunga kikapu katika mchezo huo 
   Kris Jenner, Khloe Kardashian na Kourtney Kardashian wakifurahi ushindi wa Cleveland Cavalier 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni