.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 17 Julai 2017

BALOZI SEIF AKUTANA NA BALOZI WA INDIA NCHINI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Balozi wa India Nchini Tanzania Bwana Sandeep Arya Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar {ZAWA} Dr. Mustafa Garu.
Balozi Seif akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa India Nchini Tanzania Bwana Sandeep Arya baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyomshirikisha Waziri wa Elimu Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar Dr. Mustafa Garu.
Balozi Seif wa Pili kutoka Kulia akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa India Nchini Tanzania Bwana Sandeep Arya aliyeko upende wa Kulia yake.
Wa kwanza kutoka Kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma, wa kwanza kutoka Kushoto ni Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bwana Setandar Kumar na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar Dr. Mustafa Garu.  Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana kwa mazungumzo na Balozi wa India Nchini Tanzania Bwana Sandeep Arya Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Katika mazungumzo yao yaliyohudhuriwa pia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar {ZAWA} Dr. Mustafa Garu Balozi wa India Bwana Sandeep alisisitiza umuhimu wa kuanzishwa miradi mipya itakayostawisha Jamii kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa pande hizo mbili.

Balozi Sandeep alisema India hivi sasa imejipanga kuona miradi iliyoahidi kuitekeleza kwa Tanzania ya huduma za Maji safi na Salama upande wa Zanzibar pamoja na vifaa kwa ajili ya Vituo vya kazi za amali inakamilika kwa wakati.

Alisema uimarishaji wa Vituo vya Amali utatoa nafasi kubwa kwa Vijana kupata mafunzo ya vitendo yatakayowajengea uwezo mpana wa kujipatia ajira badala ya kusubiri kutoka Serikali Kuu.

Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliishukuru Serikali ya India kwa uamuzi wake wa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar na Tanzani kwa ujumla katika kusaidia miradi ya Maendeleo.

Balozi Seif alisema Miradi ya Maji safi na Salama Visiwani Zanzibar pamoja na Msaada wa Vifaa kwa ajili ya Vituo vya Amali Nchini ni masuala ya msingi kwa wakati huu katika kuimarisha ustawi wa Wananchi.

Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimueleza Balozi huyo wa India Nchini Tanzani kwamba Zanzibar bado inaendelea kuhitaji vifaa vya Kilimo kama Matrekta kwa lengo la kusaidia nguvu za Wakulima katika sekta ya kilimo.

Balozi Seif alieleza kwamba asilimia kubwa ya Wananchi wa Zanzibar wanaendelea kutegemea Sekta ya Kilimo katoka kujipatia riziki zao na kupunguza ukali wa maisha.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
17/7/2017.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni