Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro (aliyesimama), akizungumza na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa kaskazini na Kusini Pemba (hawapo pichani) leo wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Kisiwa hicho, kulia ni Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Athuman, IGP Sirro yupo kisiwani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na watendaji wa Jeshi hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Athuman (aliyesimama), wakati akitoa neno Mbele ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Kaskazini na Kusini Pemba, IGP Sirro yupo kisiwani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na watendaji wa Jeshi hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akipokea salamu ya heshima ya kijeshi kutoka kwa Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakati akiwasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi mkoa wa Kusini Pemba leo, IGP Sirro yupo kisiwani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na watendaji wa Jeshi hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na Askari wa kikosi cha kutumia ghasi (FFU), Mara baada ya kupokea salamu ya heshima ya kijeshi, IGP Sirro yupo kisiwani Pemba kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na watendaji wa Jeshi hilo huku akiwataka askari kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha suala la uhalifu na wahalifu linadhibitiwa.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa kaskazini na kusini Pemba, wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, wakati akitoa neno kwenye kikao kazi Mara baada ya kuwasili kisiwani humo, IGP Sirro yupo kisiwani Pemba kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na watendaji wa Jeshi hilo. ( Picha zote na Demetrius Njimbwi - Jeshi la Polisi)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni