Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Jamii Media ya Tanzania inayoendesha mitandao ya JamiiForums na FikraPevu kwa kushirikiana na CIPESA(The Collaboration on International ICT Policy in East and Southern Africa) iliyo na makao makuu yake nchini Uganda imefanya Kongamano la kuwakutanisha wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini hasa wanaohusika moja kwa moja katika kulinda faragha za wateja wao ili kujadili masuala mbalimbali ya Huduma za Habari na Mawasiliano katika jukumu lao kuwa kiunganishi kati ya mteja na huduma watoazo pamoja na namna ya kulinda usiri wa taarifa za wateja wanaotumia huduma hizo.
Kabla ya kufanyika kwa Kongamano hilo siku ya Jumatano tarehe 12 Julai, Jamii Media ilifanya mafunzo ya siku mbili kuanzia tarehe 10 hadi 11 Julai kwa vijana mbalimbali wakiwemo wanasheria, wanaharakati na wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Mafunzo hayo yalilenga kujenga uelewa kuhusu sera zinazohusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Usalama wa Data Mtandaoni, Hali ya Uhuru Mitandaoni na Mambo yanayoathiri uhuru Mitandaoni nchini Tanzania.
Katika Kongamano hilo, Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Dawson Msongaleli kutoka kitengo cha Makosa ya Mtandaoni alifanya pia Uwasilishaji kuhusu Sheria ya Makosa Mtandaoni na kueleza kuwa Usiri na Usalama wa taarifa za watumiaji wa mtandao ni vitu viwili vinavyokanganya na kwamba inafika wakati ili kutekeleza kimoja inabidi misingi ya kingine ivunjwe.
Aidha, alibainisha kuwa kukosekana kwa kanuni za usimamizi wa Sheria ya Makosa ya Mtandao (The Cyber Crimes Act, 2015) ni changamoto kubwa kwani inapelekea tafsri ya Sheria hiyo kubadilika kulingana na mazingira na mtu anayetafsiri kitu ambacho kinaathiri kazi yao kama watekelezaji wa Sheria na kuahidi kuwa mamlaka zinashughulikia chamgamoto hiyo.
Mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo, Mkurugenzi wa Jamii Media, Bw. Maxence Melo alisema hili ni Kongamano la kwanza la aina hii kufanyika tangu kuanzishwa kwa JamiiForums miaka 11 iliyopita na limekuwa na matokeo chanya baada ya wadau kujadili kwa kina masuala mbalimbali yahusuyo usalama wa watumiaji.

Aliongeza kuwa wadau wengi kwenye kongamano hilo wameunga mkono hatua ya uwekaji wa sheria za kusimamia huduma nzima ya matumizi ya mitandao lakini wakashauri ufanywe kwa kutoa fursa za maendeleo na si kuminya ubunifu wala uhuru na usiri wa watumiaji wa huduma hizo.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kampuni yake itaendelea kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa huduma za mawasiliano wakiwemo wamiliki wa blogu na watumiaji wa kawaida wa mitandaonya kijamii ili kuhakikisha wanakuwa na matumizi mazuri ya huduma hiyo ili kupunguza mkanganyiko kwao na kuwapa fursa adhimu ya kunufaika na uwepo wa mitandao hiyo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni