Kaimu Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amepokea kwa mshtuko na
masikitiko makubwa msiba wa Linah George Mwakyembe - mke wa Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Linah amefariki usiku wa kuamkia
jana Julai 15, mwaka huu kwenye Hospitali ya Aga Khan alikokuwa
akipatiwa matibabu. Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa Waziri
Mwakyembe, Kunduchi jijini Dar es Salaam.
“Hakika nimeshtushwa na taarifa za
kifo cha Linah ambaye nimejulishwa kimetokea jana katika Hospitali.
Kifo hiki kimeleta huzuni kubwa kwa wanafamilia ya michezo hususani
mpira wa miguu.
“Natuma salamu za rambirambi kwako
Mheshimiwa Waziri wetu mpendwa. Hakika Nimepokea kwa masikitiko
makubwa taarifa za msiba huu. Ni pigo kubwa katika familia, lakini
kwa wakati huu mgumu, Mheshimiwa Mwakyembe, familia yake, ndugu jamaa
na marafiki hawana budi kuwa watulivu na wenye subira,” amesema
Karia.
“Naungana na familia ya Mwakyembe
katika msiba huu ambao pia ni msiba wetu sote wanafamilia ya mpira wa
miguu. Naungana nao pia kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya
Marehemu Linah Mwakyembe. Amina.”
……………………………………………………………..…………………………....................
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA
MIGUU TANZANIA
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni