Banye alianza kuimba akiwa Sunday Schools na Talent Shows lakini alivutiwa zaidi na Mwanamziki Tyrese tangu alipomuona mara ya kwanza kwenye Tangazo la Coca-Cola la mwaka 1986 na kujaribu kumfuatisha jinsi alivyoimba kila mara lile Tangazo lilipopita.
Watu wengi wakimuona kwa mara ya kwanza huwa wanahisi kama waliwahi kumuona sehemu nahisi hii ni kwasababu waliwahi kuomuona kwenye sehemu zifuatazo:-
Mwaka 2014/2015 alikuwa miongoni mwa wawashiriki 6 (Damian Soul,Grace Matata,Eli Daddy, Rogers Lucas, Myra) waliowakilisha Tanzania kwenye shindano la kuimba la Maisha Superstar nchini Kenya, kipindi hicho cha Tv kilirushwa na Maisha Magic ambapo walienda kushindana na washiriki wengine 12 kutoka nchi tofauti tofauti za Africa Mashariki, walisimamiwa na Shaa, AY(Tanzania), Jose Chameleon, Maurice Kirya (Uganda),Nameless, King Kaka(Kenya) na Music Director alikuwa Eric Wanaina.
Mwaka 2015/2016, alikuwa kati ya washiriki 5 (Nandy, Jeff, Kechu na Zouccu) waliochagulia kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano makubwa zaidi ya Karaoke kuwahi kutokea Africa, Tecno Own The Stage Lagos nchini Nigeria, kipindi hicho kilirushwa na Africa Magic Showcase ambapo pia alishindana na waimbaji wengine 14 kutoka sehemu mbalimbali za bara la Afrika.
Kwenye shindano hili walikuwa chini ya usimamizi wa Yemi Alade, MI, ID Cabasa (Nigeria), Bien Soul/Saut Sol, Anto Neosoul(Kenya) and AY (Tanzania)
Ndoto yake kubwa alitamani atoke kimuziki kupitia Mashindano ya kuimba, lakini hakuweza kufanya vizuri huko kwa sababu alikuwa anafanya multitasking…ikiwemo Shule,Kazi na Muziki kwa wakati mmoja hivyo kumpelekea kufanya maandalizi ya zima moto.
Ukiachana na Muziki Banye amesoma Masters of Business Administration in Marketing na Bachelor in Mass Communication na kaspecilize kwenye Public Relations and Marketing.
Na sasa kaamua kuingia studio na wimbo wake wa kwanza ni huo Brown Colour.
https://www.youtube.com/
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni