.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 22 Julai 2017

MJAMAICA USAIN BOLT ASHINDA MBIO ZA LIGI YA DIAMOND

Bingwa wa mara nne wa Olimpiki Usain Bolt ameshinda mbio za mita 100 katika mashindano ya ligi ya Diamond huko Monaco.

Mjamaica Bolt (30) ametumia sekunde 9.95 katika mbio zake hizo za mwisho za michuano hiyo akimshinda Mmarekani Isiah Young (9.98) na Akani Simbine (10.02) wa Afrika Kusini.

Katika mbio zingine Muingereza Laura Muir alishindwa kiurahisi na Mkenya Hellen Obiri katika mbio za mita 3,000 kwa wanawake.
Mjamaica Usain Bolt akiwa ameshika kombe la dhahabu, akiwa pia na medali yake ya dhahabu
      Mwanariadha Usain akishangilia ushindi wake akiwa na mashabiki wake wa kike

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni