Afisa Mwandamizi wa Idara ya Bajeti
wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Adam Msumule akitoa elimu ya
Bajeti kwa wananchi waliotembelea katika banda la Wizara hiyo katika
maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akipeana mkono na Balozi wa China
nchini Tanzania Dkt. LU Youqing, walipokutana katika viwanja vya
Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (sabasaba), Jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango (Mb) (kulia) akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa
Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuhusu namna ya kuongeza kasi ya
utoaji elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kukata bima ili kujikinga na
majanga, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango lilipo
katika viwanja vya maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara
(sabasaba), Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika hilo Bw. Sam Kamanga.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa
uendeshaji wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Naftal
Sigwejo baada ya kuulizwa kuhusu ubora wa baadhi ya bidhaa
zinazotolewa Serikalini baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Fedha
na Mipango katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)
Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akimpongeza Mzazi wa kijana Msuya
Mageta (katikati) aliyejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF kupitia
mpango wa Wote Scheme katika Banda la Wizara ya Fedha na Mipango
kwenye Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), Jijini Dar
es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb) (wa sita kulia) akiwa katika picha ya pamoja
na watumishi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF baada ya kutembela Banda la
Wizara hiyo katika Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia) akiwa tayari kupokea fomu ya
kujiunga kupitia mfumo wa uchangiaji wa hiari kupitia Mfuko wa
Pensheni wa PSPF kutoka kwa Msanii Mrisho Mpoto baada ya kutembelea
Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara
(Sabasaba), Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akipata maelezo kutoka Mfuko wa
Pensheni wa GEPF kuhusu huduma na mchango wa mfuko huo katika
maendeleo ya viwanda, alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika
Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akipata maelezo kutoka Banda la
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuhusu njia ya kisasa ya ufugaji Samaki
alipotembelea Banda hilo katika Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akimpongeza mtumishi wa Suma JKT
baada ya kutoa maelezo ya mtambo wa kuvuta maji katika viwanja vya
maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini-WFM)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni