.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 7 Julai 2017

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YATOA HUDUMA BURE YA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO, KUTOA USHAURI NA KUELEZA WANANCHI HUDUMA ZA MATIBABU YA MOYO WANAZOZITOA KATIKA MAONYESHO YA SABASABA

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Aika Nnkya akimpa ushauri kuhusu afya ya moyo Kizito Joseph (kushoto) ambaye alitembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
Mama Anastazia Mombeki (kulia) akipimwa urefu na Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rogers Kibula wakati alipotembelea Banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Upendo Mwaipopo akimpima mapigo ya moyo (BP) Lei Jian ambaye alifika katika banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali wanazozitoa.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Aika Nnkya akimpima mapigo ya moyo (BP) Elioth Mgulwa mkazi wa Makambako mkoani Njombe ambaye alitembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo akimpima mapigo ya moyo (BP) Mmiliki wa Bloggy ya Full Shangwe John Bukuku alitembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
Banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya banda hilo huduma zinazotolewa ni kupima magonjwa ya Moyo bure, kutoa ushauri na kueleza wananchi huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo. Picha na JKCI

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni