Mwakilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya kujitolea inayojishughulisha na masuala ya Kibinaadamu ya Umoja wa Falme za Kiarabu {UAE } ya Emirates Red Crecent Bwana Said Al – Khemeir alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
Bwana Said alisema Uongozi wa Taasisi yake ulifika Zanzibar kuangalia maeneo yaliyoathirika na Mvua hizo na kuandaa Mipango itakayosaidia kuanzwa kwa Mradi huo mkubwa utakaohusisha Wilaya zote zilizopatwa maafa hayo.
Alisema Awamu ya kwanza ya mradi huo itaanza Kisiwani Pemba kwa ujenzi wa Nyumba 30, zitakazokuwa na uwezo wa kuchukuwa Familia Mbili, Skuli yenye Madarasa Saba na Maktaba yake, Hospitali, Msikiti pamoja na Maduka kwa ajili ya wakaazi watakaoishi eneo husika.
Mwakilishi huyo wa Taasisi ya Kimataifa ya kujitolea inayojishughulisha na masuala ya Kibinaadamu ya Emirates Red Crecent alisema Taasisi hiyo yenye kufanya kazi chini ya ushauri wa Vyama vya Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwekundu Duniani imekuwa ikitoa huduma za kibinaadamu katika Mataifa mbali mbali Duniani kutegemea na mahitaji ya Nchi husika.
Naye Mhandisi Muandamizi wa Taasisi hiyo ya Emirates Red Crecent Fateh Basel aliishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwamba maeneo yatakayotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba hizo ni vyema yakawa salama.
Mhandisi Basel alisema maeneo yatakayotengwa endapo yatakuwa karibu na miundombinu ya Bara bara, Maji na Huduma za Umeme yatasaidia kurahisisha mradi huo kukamilika kwa haraka ili kutoa faraja kwa Wananchi waliothirika na Mvua za masika zilizopita.
Aliupongeza ushirikiano wa karibu ulioonyeshwa na watendaji wa Wilaya na Mikoa wakati wa ziara yao ya kukagua sehemu zilizoathirika na Mvua za Masika pamoja na kuangalia baadhi ya maeneo salama yenye sifa na haiba ya kujengwa kwa mradi huo.
Akitoa shukrani zake kwa Uongozi wa Taasisi hiyo ya Emirates Red Crecent Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kitendo kilichobuniwa na Taasisi hiyo hakitolea faraja kwa Wananchi walioathirika na janga hilo pekee bali hata na Serikali Kuu kwa ujumla.
Balozi Seif alisema atauagiza Uongozi wa Kila Mkoa na Wilaya Visiwani Zanzibar kufanya utafiti na uhakiki wa kuangalia maeneo yatakayoweza kuanzishwa miradi hiyo itakayostawisha Wananchi waliokusudiwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhakikishia Uongozi huo wa Emirates Red Scecent kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itazingatia wazo hilo kwa ajili ya kulitolea baraka zake ili Mradi huo uanze mara moja na kulet tija iliyokusudiwa.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
21/7/2017.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akisalimiana na Mwakilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya kujitolea inayojishughulisha na masuala ya Kibinaadamu ya Umoja wa Falme za Kiarabu {UAE } ya Emirates Red Crecent Bwana Said Al – Khemeir.
Wa kwanza kutoka Kulia ni Mhandisi wa Taasisi ya Emirates Red Crecent Bwana Fateh Basel.
Balozi Seif akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wa Taasisi ya Kimataifa ya kujitolea inayojishughulisha na masuala ya Kibinaadamu ya Umoja wa Falme za Kiarabu {UAE } ya Emirates Red Crecent Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Mwakilishi wa Taasisi ya Emirates Red Crecent ya Umoja wa Falme za Kiarabu Bwana Said Al – Khemeir wa Pili kutoka Kushoto akimfafanua Balozi Seif nia ya Taasisi yake kujenga Nyumba kwa ajili ya Wananchi walioathirika nja Mvua za Masika.
Mhandisi wa Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation Bwana Khamis Rasshid wa kwanza kutoka Kulia ambaye Kampuni yake ndio itakayosimamia Ujenzi wa Nyumba za Wananchi walioathirika na Mvua za Masika akifafanua jambo wakati Ujumbe wa Emirates Red Crecent upofanya mazunguma na Balozi Seif.
Bwana Said Al – Khemeir akimuonyesha Balozi Seif ramani za Majengo ya nyumba zintakazojengwa na Emirates Red Crecent hapa Zanzibar kwa ajili ya Wananchi walioathirika na Mvua za Masika.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Emirates Red Crecent pamoja na ule wa Milele Zanzibar Foundation mara baara kumaliza mazungumzo yao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni