.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 22 Agosti 2017

WANANAUME WANNE AFRIKA KUSINI KIZIMBANI KWA KULA NYAMA YA BINADAMU

Wanaume wanne Afrika Kusini wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na makosa ya kula nyama za watu, baada ya mmoja wao kujipeleka mwenyewe katika kituo cha polisi na kusema amechoka kula nyama za binadamu.

Polisi walipomhoji mtu huyo aliwaonyesha mguu wa mtu na mkono wa mtu na ndipo walipoenda naye kwenye nyumba yake iliyopo KwaZulu-Natal, ambapo miili zaidi ya watu ilipatikana na kuwakamata wanaume hao wakiwemo waganga wawili wa jadi.

Msemaji wa polisi ameviambia vyombo vya habari imesema wanaume hao wanne wanaumri wa miaka kati ya miaka 22 na 32 ni sehemu ya genge kubwa la wala watu.

Uchunguzi bado unaendelea huku Polisi wakiwahimiza watu ambao ndugu zao wamepotea wajitokeze.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni