.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 21 Oktoba 2017

HUDDERSFIELD TOWN YAWA TIMU YA KWANZA KUIFUNGA MAN U LIGI KUU YA UINGEREZA

Timu ya Huddersfield Town imemaliza rekodi ya Manchester United ya kutofungwa katika Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu kwa kuipa kipigo cha kwanza cha magoli 2-1.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la John Smith's Manchester United walifungwa goli la kwanza baada ya Juan Mata kupoteza mpira ulionaswa na Aaron Mooy.

Mooy aliambaa na mpira huo na kumpasia kiungo Tom Ince aliyepiga mpira uliookolewa na kipa David de Gea, na mpira huo kumkuta Mooy akaupachika wavuni.

Uzembe wa beki Victor Lindelof uliizawadia Huddersfiel goli la pili lililofungwa na Laurent Depoitre, huku Marcus Rashford aliyetokea benchi akifunga goli pekee la Manchester United.
              Laurent Depoitre akimzunguka kipa Davidi De Gea na kufunga goli la pili
  Marcus Rashford akiuunganisha kwa kichwa mpira uliopigwa na Romelu Lukaku na kufunga goli pekee la Manchester United

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni