Madaktari bingwa wa upasuaji nchini
India katika Jiji la Delhi wamefanikiwa kuwatenganisha watoto mapacha
walioungana vichwa.
Watoto hao wa mwaka mmoja waitwao
Jaga na Kalia wamefanyiwa upasuaji kwa muda wa saa 16, na kwa sasa
wapo kwenye chumba cha wagonjwa mahututi, kwa mujibu wa madaktari.
Timu ya madaktari 30 waliofanya
upasuaji huo wote wanatoka Taasisi ya Sayansi ya Tiba ya nchini
India.
Watoto hao mapacha wanaume
walizaliwa wakiwa wamechangia mishipa ya damu na mishipa midogo ya
kwenye ubongo.
Mmoja wa watoto mapacha walioungana kichwani akiwa amelala baada ya kutenganishwa


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni