Kwa msaada huu, tunawezesha uchukuaji hatua unaoendana na sera ya nje inayozingatia haki za wanawake ya Uswidi na pia jitihada zinazolenga, miongoni mwa mambo mengine, ajira yenye hadhi na haki za watoto. Hii inadhihirisha mwendelezo wa uhusiano wa karibu na Umoja wa Mataifa na serikali ya Tanzania wenye lengo la kuleta maendeleo yenye usawa na jumuishi zaidi,” alisema Balozi.
Akisisitiza utayari wa kuendelea kuisaidia Tanzania na Umoja wa Mataifa, Balozi alitumia fursa hiyo kuthibitisha kuyapokea kwa moyo mmoja mageuzi ya Mfumo wa UN chini ya Mpango wa Kufanya Kazi Pamoja na kutambua njia fungamanifu zinazotumika na thamani inayopatikana kutokana na mchango wa mashirika ya UN katika lengo moja kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania, washirika wa kijamii na vyama vya kiraia.
Akizungumza baada ya kutiliana saini makubaliano, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Rodriguez alitoa shukrani kwa serikali na watu wa Uswidi kwa msaada wao endelevu akiipongeza Uswidi kwa kuwa mshirika wa maendeleo asiyeyumba katika shughuli za Umoja wa Mataifa Moja na pia kwa Tanzania.
“Uswidi imekuwa mshirika wa kuaminika wa Tanzania na Umoja wa Mataifa kwa miongo mingi. Kwa kulenga wale walio wanyonge kabisa katika jamii hii, rasilimali hii itatoa mchango muhimu sana katika kushughulikia mahitaji ya wale ‘walio chini sana’ kama inavyoelekezwa katika Malengo ya Ulimwengu,” alisema.“Mchango huu utauwezesha Umoja wa Mataifa kuweza kufanya kazi katika masuala mapana mengi kama vile kuhamasisha fursa za ajira zenye hadhi kwa Watanzania maskini, kuendeleza kanuni za utawala bora, na nafasi ya uongozi wa wanawake katika masuala ya siasa na vilevile kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,” aliongeza.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni