Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka Paul Kessy wakati akifungua mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF).
Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuangalia mada tatu zilizokubaliwa kufanywa kama sehemu ya kutengeneza mwongozo wa namna ya kuendesha mpango huo ili kuisaidia serikali katika kutengeneza miji salama na yenye tija.
Mada hizo tatu ni pamoja na kuangalia miundombinu ya miji na huduma za kifedha katika utengenezaji wa miji, mahusiano ya serikali kuu na ya mitaa ; na mada ya tatu ni namna ya kupata taarifa sahihi ili kuimarisha uwekezaji.
Kessy alisema wakati serikali inatekeleza malengo ya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano (FYDP) ll , wenye lengo la kuweka mazingira sawa kwa uchumi wa viwanda na maendeleo, mpango huo wa ESRF umekuja muda muafaka kwani utasaidia kutafuta na kutoa majawabu halisi na sahihi.
Alisema kwamba kama nchi itataka kuwa na maendeleo yenye kujali binadamu ni vyema kuwa na maamuzi ya miongo yenye kuakisi uhalisia na mahali pekee kwa sasa kupata huo uhalisia ni wa kutumia mpango huo wa ESRF ambapo wanazuoni watakutana kujadili uhalisia wa mambo na kutoa mapendekezo ya kukabili changamoto.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk Tausi Kida alisema mkutano huo ambao ni wa kwanza tangu alipoamua kuwa na Tanzania Urbanisation Laboratory, Agosti mwaka huu umelenga kusaidia kutengeneza njia ya kusaidia utengenezaji wa miji salama yenye tija nchini.
Alisema kwa kuwa mwenyekiti wa mpango huo ni Tume ya Mipango wao wakiratibu tu, ni dhahiri mawazo na mapendekezo yatakayokuwa yanatolewa kulingaana na utafiti yatasaidia sana kuwa na miji salama.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni