Kocha wa Manchester City, Pep
Guardiola, amesema kujiamini kwa Raheem Sterling kumemfanya awe na
kiwango bora baada ya kufunga goli la ushindi dhidi ya Southampton
katika dakika ya 96.
Goli hilo la Sterling ni la 13
katika msimu huu na limeipa klabu yake ushindi wa 12 katika msimu huu
wa Ligi Kuu na kuongoza kwa tofauti ya pointi nane, baada ya mchezo
huo kuisha kwa magoli 2-1.
Mchezaji Oriol Romeu akishangilia baada ya kufunga goli na kufanya matokeo kuwa 1-1
Raheem Sterling akiifungia Manchester City goli la pili na la ushindi katika dakika za ziada
Kocha wa Chelsea Antonio Conte
amemuomba radhi refa Neil Swarbrick baada ya kutolewa nje kwa kupinga
maamuzi ya refa katika mchezo ambao Chelsea ilipata ushindi kiduchu
wa goli moja.
Kocha huyo raia wa Italia alijikuta
katika kipindi chote cha pili akiangalia mchezo huo katika dimba la
Stamford Bridge kwa kutumia runinga akiwa katika chumba cha
kubadilishia nguo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni