Hafla ya uzinduzi wa Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake imezinduliwa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe kwenye Uwanja wa General Tyre jijini Arusha.
Timu zilizokata utepe zilikuwa ni Alliance Queens ya Mwanza iliyoshinda mabao 2-1 dhidi ya Panama FC ya Iringa.
Katika uzinduzi huo Waziri Dk. Mwakyembe aliwataka wachezaji wa timu zote kujituma kwa juhudi zaidi kwa kuwa mpira wa miguu kwa sasa ni ajira kubwa sana kwa vijana.
“Vijana wangu natambua mnapenda mpiwa wa miguu, naomba mzingatie vitu vitatu muhimu - nidhamu, juhudi na kujitunza,” amesema Waziri Dk. Mwakyembe akiwa na Rais wa TFF Wallace Karia, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred na viongozi wa FA Mkoa wa Arusha.
Mara baada ya kufanya uzinduzi huo, Waziri akiwa na viongozi hao leo ametembelea Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kutazama maendeleo ya marekebisho yanayofanyika kwenye Uwanja huo.
Mbali na uwanja huo pia waziri alifanya ziara fupi kwenye viwanja wmbalimbali ikiwa ni pamoja na kiwanja cha FFU kwa Morombo, Arusha ambapo aliwapongeza kwa ukarabati mzuri wa nyasi za kuchezea.
Katika ziara nyingine Waziri pamoja na Viongozi wa TFF walitembelea shule ya Trust St. Patric Sports Academy ambacho ni kutuo cha kukuza michezo na timu zinazoshiriki ligi hiyo, zimeweka kambi.
WAAMUZI 18 TANZANIA WATAPA BEJI FIFA 2017/18
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu Tanzania (FIFA), limetoa beji kwa Waamuzi 18 katika msimu wa mshindano mwaka 2018.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka FIFA, Waamuzi walioteuliwa kwa upande wa wanaume ni Mfaume Ali, Elly Sasii, Emmanuel Mwandembwa na mkongwe Israel Nkongo na kwa upande wa wanawake wamo Jonesia Rukyaa na Florentina Zablon.
Waamuzi Wasaidizi walipewa beji hizo (Wanaume) ni Soud Lillah, Mgaza Kunduli, Mohammed Mkono, Mbaraka Haule, Ferdinand Frank Chacha na Frank Komba na kwa wanawake Hellen Mduma, Dalila Jaffari, Jeneth Balama na Grace Wamala.
Waamuzi wa mpira wa miguu unaochezwa ufukweni waliopata beji ni Jackson Steven Msilombo na Geofrey Tumaini Mwamboneko.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni