.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 28 Novemba 2017

RAIS KENYATTA AAPISHWA NA KUTANGAZA NEEMA KWA WAKENYA NA WANA EAC

Rais Uhuru Kenyatta ameapa kushughulikia mgawanyiko uliopo nchini Kenya wakati akiapishwa kwa muhula wa pili, katika sherehe ambazo zilisusiwa na kambi ya upinzani nchini Kenya.

Akiongea baada ya kuapishwa katika uwanja wa Kasarani Jijini Nairobi mbele ya maelfu ya wananchi wafuasi wa chama chake, rais Kenyatta amesema atachukua baadhi ya mawazo ya wapinzani katika kuonyesha ushirikishwaji.

Rais Kenyatta ameahidi, kufufua moyo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwamba wananchi wa EAC watahesabiwa kama Wakenya na watahitaji kutumia kitambulisho pekee kuingia ama kutoka pamoja na kufanya kazi, kumiliki mali au hata kuoana bila kuwekewa masharti.

Aidha, amesema kuanzia Desemba mwaka huu gharama za umeme zitapunguzwa usiku, kwa 50% kati ya saa nne usiku hadi alfajiri na kuongeza kuwa katika kipindi cha mwisho cha miaka yake mitano atahakikisha Wakenya milioni 13 wanapata huduma ya afya kwa 100% kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF.

Sherehe za kuapishwa kwa Rais Kenyatta zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Afrika akiwemo rais Salva Kiir wa Sudan Kusini, Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalign, rais Paul Kagame wa Rwanda ambapo Tanzania iliwakilishwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.

Baada ya sherehe hizo mpinzani wake Mkuu Raila Odinga amehutubia wafuasi wake huko Langata na kusema anaandaa mipango ya kuapishwa kama rais mwezi ujao. Hata hivyo mkutano huo ulisambaratishwa na polisi kwa mabomu ya machozi.
       Sehemu ya wananchi wa Kenya waliojitokeza kushuhudia kuapishwa rais Uhuru Kenyatta

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni