.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 7 Novemba 2017

WAZIRI MHAGAMA AKUTANA NA WADAU WA MASUALA YA AJIRA NA UKUZAJI UJUZI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisisistiza jambo kwa wajumbe wa Kikao cha wadau wa masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kilichofanyika Mjini Dodoma Novemba 7, 2017.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Erick Shitindi akisisitiza jambo kuhusu mkakati wa Serikali kuboresha mazingira ya Ajira hapa nchini walipokutana leo Mjini Dodoma katika kikao cha Wadau wa masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw .Geodfrey Simbeye akisisitiza jambo wakati wa Kikao cha pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Kikao cha kujadili masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa akichangia mada kuhusu ushiriki wa watu wenye ulemavu katika programu zinazotekelezwa na Serikali katika masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi ili kujikwamua kiuchumi.
Wajumbe wa kikao cha kujadili masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa kikao cha Kujadili Masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kilichofanyika Mjini Dodoma.
Meneja wa Maendeleo ya Biashara na Huduma Bi Jane Gonsalves akichangia hoja kuhusu mikakati ya Serikali kuwawezesha Vijana kupata ajira na kujiajiri wakati wa kikao cha kujadili masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi leo Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akichangia hoja kuhusu namna bora ya kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi wakati wa kikao cha Kujadili masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi Novembna 7, 2017 Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Dkt.Aggrey Mlimuka akichangia hoja wakati wa kikao cha kujadili masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU – DODOMA)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni