Kinda Justin Kluivert ameionyesha
Manchester United kipaji chake baada ya kuisaidia Ajax kushinda kwa
magoli 3-1 dhidi ya Willem II ikicheza bila Marcel Keizer na Dennis
Bergkamp.
Kikosi cha Ajax Amsterdam
kilitandaza soka safi dhidi ya Willem II, huku Kluivert akifunga
goli la kusawazisha na kisha Kasper Dolberg na David Neres kuongeza
mengine.
Kluivert ambaye ni mtoto wa Mholanzi
Patrick, Kluivert amefunga magoli matano msimu huu na kocha wa United
Jose Mourinho ni miongoni mwa makinda wanaomvutia.
Mpira uliopigwa na kinda Justin Kluivert ukimshinda kipa wa Willem na kujaa wavuni


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni