.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 13 Desemba 2017

SHIRIKA LA WOTE SAWA LABAINI IDADI KUBWA YA WATOTO WANAOAJIRIWA MAJUMBANI

Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani WOTESAWA, Angel Benedicto amesema kasi ya watoto kuajiriwa kufanya kazi za nyumbani inazidi kuongezeka Jijini Mwanza.

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na shirika la WOTESAWA katika Kata nne za Manispaa ya Ilemela ambazo ni Kitangiri, Kawekamo, Nyasaka na Kiseke umebaini watoto zaidi ya 400 walioajiriwa kufanya kasi za nyumbani.

Hata hivyo shirika hilo kupitia mradi wake wa Paza Sauti ya Mfanyakazi wa Nyumbani unaofadhiliwa na Shirika la The Voice kupitia serikali ya Uholanzi, limeanza kutoa elimu kwa viongozi wa serikali za mitaa wakiwemo Madiwani, Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Mitaa, waajiriwa wa kazi za nyumbani pamoja na waajiri wao ili kupambana na hali hiyo katika Kata tajwa hapo juu ambazo zinanufaika na mradi huo
Mkurugenzi wa WOTESAWA, Angel Benedicto (kushoto) akizungumza na mwandishi wa DW, Hawa Bihoge hii leo.

Rehema Mkinza ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Ilemela akizunguza na mwandishi wa DW, Hawa Bihoge kuhusiana na hali ya watoto wafanyakazi wa nyumbani.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni